• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya China nchini Uganda yatengeneza simu za kisasa zenye kipimajoto ili kupambana na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-08-12 09:51:41

    Kampuni ya ENGO ya China iliyoko nchini Uganda imeanza kutengeneza simu za kisasa zenye uwezo wa kupima joto la mwili.

    Kampuni hiyo iliyoko wilaya ya Mukono imeliambia Shirika la Habari la China Xinhua kuwa, uvumbuzi huo ni muhimu kwa biashara baada ya miezi minne ya kufungwa kwa shughuli za biashara nchini Uganda.

    Katibu wa mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo David Beecham Okwere amesema, utengenezaji wa simu hiyo umetumia kipindi cha miezi minne kwa kuungwa mkono na kampuni mama iliyoko China. Ameongeza kuwa simu hiyo kwa sasa inafanyiwa mchakato wa ukaguzi wa viwango na Mamlaka ya Viwango nchini Uganda, na kuongeza kuwa majaribio ya awali yameonyesha kuwa simu hiyo inaweza kupima joto la mwili kwa usahihi bila kuwa na muda wa kusubiri.

    Waziri wa nchi anayeshughulikia uwekezaji wa Uganda Bi. Evelyn Anite amesea, maendeleo hayo ni habari njema kwa Uganda na Afrika, hususan wakati huu ambapo maambukizi ya virusi vya Corona yanaongezeka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako