• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Gazeti la Daily Trust la Nigeria lachapisha makala ya kukanusha nadharia ya "mtego wa madeni" wa China

    (GMT+08:00) 2020-08-12 17:26:22

    Gazeti maarufu la Daily Trust la Nigeria hivi karibuni limechapisha makala ya kukanusha nadharia ya "mtego wa madeni" unaotokana na mikopo ya China.

    Makala hiyo inasema, shutuma zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari vya Nigeria kuwa makubaliano ya mikopo yaliyosainiwa kati ya serikali ya Nigeria na China yanaharibu mamlaka na uhuru wa Nigeria, hazina msingi wowote. Makala hiyo imebainisha kuwa China na Nigeria ni wenzi wa ushirikiano wanaoshirikiana kwa hiari kutokana na maslahi yao ya pamoja. Nigeria inaagiza bidhaa nyingi kutoka China, na pia ni nchi ya pili inayowekezwa zaidi na China barani Afrika, kwa hivyo kuendeleza na kupanua ushirikiano na China ni chaguo bora kwa Nigeria kwa sasa.

    Makala hiyo imesisitiza kuwa, Nigeria na nchi nyingine za Afrika zinapaswa kutumia maliasili yake kwa hatua mwafaka, kuboresha muundo wa uchumi na kuchochea ukuaji, ili kuweza kutimiza maendeleo endelevu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako