• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda kuwa mfano wa kuigwa wa kupambana na virusi vya Corona Afrika

    (GMT+08:00) 2020-08-12 18:55:39

    Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO Dk. Tedros Adhanom Gebreyesus hivi karibuni ametaja baadhi ya nchi na sehemu zilizofanikiwa kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona, ikiwemo Rwanda.

    Kwa mujibu wa wizara ya afya ya Rwanda, hadi kufikia jana Jumanne, nchi hiyo imethibitisha maambukizi 2,171 ya virusi vya Corona, ambayo kati yao wagonjwa 1,478 wamepona na watu saba wamefariki dunia.

    Dk. Tedros amesema mafanikio yaliyopatikana Rwanda yanatokana na uongozi imara, upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi wote, uungaji mkono mkubwa kwa wafanyakazi wa afya na usambazaji wenye ufanisi wa taarifa za afya ya umma.

    Wataalamu wanaona kuwa, serikali ya Rwanda imeonesha nia thabiti ya kupambana na virusi vya Corona, na kuhakikisha hatua za kudhibiti janga la virusi hivyo zinatekelezwa ipasavyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako