• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan kupeleka polisi kwenye jimbo la Bahari Nyekundu ambapo mapambano ya kikabila yanaendelea

    (GMT+08:00) 2020-08-13 08:54:08

    Baraza la Mawaziri nchini Sudan jana limetangaza uamuzi wake wa kupeleka jeshi la polisi kwenye jimbo la Bahari Nyekundu, mashariki mwa nchi hiyo, ambapo mapambano ya kikabila yanaendelea.

    Takwimu zisizo za kiserikali zinadai kuwa, watu zaidi ya 25 wameuawa tangu Jumapili mapambano yalipotokea kati ya makabila ya Bani Amer na Al-Nuba kwenye Bandari ya Sudan.

    Habari nyingine zimesema, taarifa iliyotolewa jana na mkutano wa nane wa Marafiki wa Sudan imesisitiza umuhimu na uungaji mkono kikamilifu kwa utulivu wa Sudan.

    Taarifa hiyo pia imesisitiza kuiunga mkono serikali ya mpito ya Sudan inayoongozwa na waziri mkuu Abdalla Hamdok, na kusifu uongozi wake katika kuzingatia amani kamili na ya umoja, licha ya nchi hiyo kukabiliwa na changamoto za janga la COVID-19.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako