• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika CDC yatoa wito wa uratibu zaidi ili kudhibiti janga la COVID-19 barani Afrika

    (GMT+08:00) 2020-08-13 09:37:59

    Mkurugenzi wa Kituo cha Kudhibiti na Kukinga Magonjwa cha Afrika (Africa CDC) John Nkengasong ametoa wito wa uratibu zaidi wa kikanda na kimataifa ili kudhibiti kasi ya kuenea kwa virusi vya Corona barani Afrika.

    Akizungumza na Shirika la Habari la China Xinhua, Nkengasong amesisitiza haja ya kufanya kazi chini ya kanuni za ushirikiano, uratibu na uhusiano barani Afrika na kimataifa. Pia ameisifu serikali ya China na kampuni zake kwa kuiunga mkono Afrika katika mapambano yake dhidi ya virusi vya Corona. Nkengasong pia amesisitiza kuwa bara la Afrika linahitaji maboksi milioni 15 ya kufanyia vipimo kwa mwezi ili kuweza kukabiliana na janga hilo.

    Takwimu zilizotolewa na Kituo hicho zimeonyesha kuwa, mpaka kufikia jana jumatano, idadi ya kesi zilizothibitishwa kuwa na virusi vya Corona barani Afrika zilifikia 1,064,546, huku idadi ya vifo ikiongezeka na kufikia 23,839, na idadi ya watu waliopona virusi hivyo pia imeongezeka na kufikia 758,292.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako