• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zambia yaishukuru China kwa kuunga mkono miradi yake ya maendeleo

    (GMT+08:00) 2020-08-13 09:38:22

    Serikali ya Zambia imeishukuru China kwa kuunga mkono miradi yake ya maendeleo kwa miaka kadhaa na kusaidia ajenda ya maendeleo ya nchi hiyo.

    Akizungumza kwenye mkutano wa ngazi ya juu wa timu ya pamoja ya China na Afrika katika kukabiliana na janga la virusi vya Corona uliofanyika kwa njia ya video, Balozi wa Zambia nchini Ethiopia Emmanuel Mwamba ambaye pia ni Mwakilishi wa Kudumu wa Zambia kwenye Umoja wa Afrika amesema, Zambia itaendelea kuishukuru China kwa kuiunga mkono kifedha, kiteknolojia na kwa vifaa uliotolewa kwa miaka kadhaa, na kwa uungaji mkono hivi karibuni wa vifaa tiba ili kupambana na janga la virusi vya Corona.

    Balozi Mwamba ameitaka China na wenzi wengine kuiunga mkono Zambia kwa kuipatia vifaa vinavyohitajika ikiwemo vifaa vinavyotakiwa kupambana na janga hilo ikiwemo vifaa vya utambuzi, na upimaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako