• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona barani Afrika yazidi milioni 1.06

    (GMT+08:00) 2020-08-13 16:42:29

    Takwimu mpya zilizotolewa jana na Kituo cha Kinga na Udhibiti wa Magonjwa cha Afrika (Africa CDC) zinaonesha kuwa, idadi ya maambukizi yaliyothibitishwa ya virusi vya Corona kote barani Afrika imefikia 1,066,505, na idadi ya vifo vinavyotokana na virusi hivyo imefikia 23,886.

    Kwa mujibu wa Africa CDC, maambukizi ya virusi vya Corona yanaenea kwa kasi nchini Namibia, Zimbabwe na Kenya, na baadhi ya nchi za Afrika zimechukua hatua kali zaidi za kinga na udhibiti dhidi ya virusi hivyo.

    Rais Hage Geingob wa Namibia jana Jumatano alitangaza hali ya dharura ya kitaifa itakayodumu kwa siku 16 kuanzia leo, kutokana na kuongezeka kwa kasi kwa maambukizi ya virusi vya Corona nchini humo.

    Nchini Zimbabwe, madaktari na wauguzi 70 wa Kituo cha Tiba ya Virusi vya Corona cha Hospitali ya Parirenyatwa mjini Harare wamethibitika kuambukizwa virusi hivyo, na wengi wao wamelazimika kupewa matibabu au kuwekwa karantini nyumbani.

    Jana Jumatano idadi ya maambukizi mapya ya virusi vya Corona nchini Kenya ilifikia 679. Mwakilishi wa WHO nchini Kenya Dk. Rudi Eggers amesema baadhi ya wakenya kutofuata hatua za kinga na udhibiti kama vile kuvaa barakoa, kudumisha umbali wa kijamii na kunawa mikono mara kwa mara, kumechangia kuongezeka kwa maambukizi hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako