• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Namibia yatiwa moyo na juhudi za China katika kutafuta chanjo ya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-08-13 18:50:38

    Waziri wa Afya na Huduma za Jamii wa Namibia Kalumbi Shangula amesema nchi yake inatiwa moyo na juhudi za China katika kutafuta chanjo ya COVID-19.

    Akijibu maswali Ikulu jana Bw. Shangula amesema kuna juhudi nyingi zinazofanywa hasa na China katika kutafuta chanjo, na hata Russia nayo pia inajitahidi. Aidha amebainisha kuwa Namibia inataka kupata ufumbuzi wa kudumu, pamoja na chanjo ya COVID-19, na kwamba nchi kwa sasa inashughulikia kupunguza athari za muda mrefu za janga hili.

    Namibia imekuwa ikishuhudia kuongezeka kwa kasi kwa maambukizi ya COVID-19 hasa katika mji mkuu wake Windhoek, ambapo wataalamu wa afya wanasema mji huo karibuni utakuwa kitovu cha mlipuko wa virusi vya Corona nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako