• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda: Uuzaji wa sukari nje ya taifa wadidimia kwa asilimia 54.

  (GMT+08:00) 2020-08-17 16:54:57
  Mapato ya kuuza sukari nje ya Uganda yamepungua kwa asilimia 54 huku mataifa jirani yakifungia bidhaa hii kutoingizwa masokoni mwake.

  Kulingana na benki ya Uganda, kufikia mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu, mapato ya sukari kwa Uganda yalipungua hadi dola milioni 7.4 kutoka dola milioni 11.4 mwezi wa Mei mwaka huu. Katika kipindi hiki, Uganda iliuza jumla ya tani 14,991 ya sukari, kutoka tani 23,212 mwezi Mei.

  Huu ulikuwa upungufu wa takriban tani 8,221, ikiwa ni asilimia 54 chini. Wasomi wa masuala ya uchumi wanasema kwamba huenda hali ikawa mbaya zaidi endapo Uganda haitatatua mizozo ya kibiashara iliyopo na mataifa jirani.

  Mwezi uliopita, Kenya ilifutilia mbali vibali vya wanaoagiza sukari kutoka uganda, kwa madai kwamba soko lake limejaa sukari ya bei ya chini sana. Waziri wa Kilimo wa Kenya Peter Munya, alisema kwamba hii inahatarisha sekta ya kilimo cha miwa nchini Kenya na kuwapa hasara wakulima wa zao hilo. Hadi siku za hivi punde, Kenya imekuwa mnunuzi mkuu wa suakri kutoka Uganda. Kufutiliwa mbali kwa vibali vya wanaoagiza sukari hii, kuna maana kwamba Uganda haitauza takriban tani 35,000 ya sukari kwa kenya.

  Tanzaia haijachukuwa sukari ya Uganda tangu mwezi Juni. Kiwango cha mwisho cha sukari kununulia na Tanzania kutoka Uganda, kilikuwa tani 20,000 mwezi huo wa Juni.

  Tayari Uganda inatafuta mbinu za kuza sukari yake nje ya Afrika Mashariki. Mataifa yanayolengwa sana ni DR Congo, Sudan Kusini, Ethiopia na Zambia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako