• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Inter Milan waingia fainali ya Ligi ya Europa baada ya kuwaadhibu Shakhtar Donetsk.

    (GMT+08:00) 2020-08-18 19:16:51

    Timu ya Inter Milan inayoongozwa na Antonio Conte imefanikiwa kuingia fainali ya kombe la Europa, baada ya kuifunga timu ya Shakhtar Donetsk kwa jumla ya magoli matano kwa bila. Inter iliongoza katika nusu ya kwanza kwa goli moja lililofungwa na Lautaro Martínez, na katika kipindi cha pili mvua ya magoli ikaendelea kunyesha baada ya Danilo D'ambrossio kuongeza goli moja, na Martinez kuongeza goli lingine, kabla ya Lukaku kutingisha nyavu mara mbili. Lukaku ambaye alitimkia Italia kutoka Uingereza sasa ameifungia timu yake magoli 8 kwenye 10 za mwisho alizocheza kwenye mashindano mbalimbali. Kwenye fainali ya Europa ligi timu zitakazokutana ni Sevilla ya Hispania waliowatoa Man United, watakaocheza dhidi ya Inter milan. Na Man United na Shakhtar Donetsk watakutana ijumaa hii katika mechi ya kutafuta mshindi wa tatu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako