• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Paris Saint Germain ya Ufaransa yaingia fainali ya klabu bingwa Ulaya

    (GMT+08:00) 2020-08-19 16:53:18

    Baada ya kutofanya vizuri kwenye ligi ya Ulaya kwa zaidi ya muongo mmoja sasa, Klabu ya Paris saint Germain ya Ufaransa sasa imefika kwenye kilele cha ligi za ulaya baada ya kufanikiwa kuingia kwenye fainali inayotarajiwa kuchezwa jumapili hii, dhidi ya mshindi kati ya Bayern Munich ya Ujerumani na Lyon ya Ufaransa. Alikiwa ni Angel Di Maria aliyefunga goli moja na kusaidia mawili katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Rasen Ballsport Leipzig ya Ujerumani kwenye mchezo wa Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya uliofanyika jana usiku katika uwanja wa Luz Jijini Lisboa, nchini Ureno. Di Maria alifunga bao lake katika dakika ya 42 baada ya kumsetia Marquinhos kufunga la kwanza dakika ya 13, na Juan Bernat kufunga la tatu dakika ya 56. Timu ya Leipizig ambayo iliundwa miaka 11 iliyopita haina uzoefu mkubwa kwenye mashindano ya kimataifa, na kwenye mchezo wa jana wengi walinipigia upatu PSG iliyosheheni nyota wakubwa kama kina Mbappe, Neymar, Di-maria na wengine wengi, ambao walicheza bila kuonyesha ubinafsi hata kidogo na kujipatia ushindi huo mnono. Leo mtambo mwingine wa Ujerumani Bayern Munich unapigiwa upatu zaidi kwenye mechi dhidi ya Lyon, lakini hadi dakaika hii inaonekana kama huu ni mwaka wa wafaransa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako