• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Klabu ya Sofapaka yawasajili Roy Okal na Kevin Omondi

    (GMT+08:00) 2020-08-20 19:09:58

    Klabu ya Sofapaka FC ya Kenya imethibitisha kuwasajili Roy Okal na Kevin Omondi kutoka Mathare United na Wazito FC, ikiwa ni sehemu ya hatua za kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya ligi kuu ya Kenya. Okal ni mchezaji wa kiungo na Omondi ni mlinda mlango na wote wamesajiliwa kwa mikataba ya miaka miwili. Okal mwenye umri wa miaka 24 alikuwa mwanafunzi wa Laiser Hill ambaye alionyesha umaarufu wakati wa mashindano ya taifa ya shule za sekondari ambapo anatarajiwa kujaza nafasi ya Cercidy Okeyo ambaye amekwenda kutafuta mkate wake Mashariki ya Kati baada ya mkataba wake na Sofapaka kumalizika. Okal amewahi kuchezea Ushuru na klabu moja ya Ugiriki ya daraja la chini. Omondi kwa upande wake atajaza nafasi ya mlindamlango Mganda, Nicholas Sebwato aliyeondoka baada ya mkataba wake kumalizika, lakini atalazimika kuwania nafasi na Richard Aimo pamoja na Isaiah Wakasala.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako