• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kocha mpya Yanga Cedric Kaze aanza kazi kimya kimya

    (GMT+08:00) 2020-08-20 19:10:27

    Wakati mashabiki wa Klabu ya Yanga wakiendelea kusubiri kwa hamu kumjua na kumuona kocha mkuu wa kikosi hicho, mazoezini tayari wachezaji wa timu hiyo wameanza kuzifaidi mbinu na mfumo wa kocha huyo ambaye atatambulishwa rasmi mwishoni mwa wiki hii. Yanga ambayo kwa muda mrefu imekuwa sokoni kutafuta kocha mkuu wa kurithi mikoba ya Mbelgiji Luc Eymael aliyetimuliwa baada ya kumalizika msimu wa 2019/20, imeanza mazoezi ikiwa chini ya Kocha wa viungo, rai wa Afrika Kusini, Riedoh Berdien. Ingawa mashabiki wa soka wamekuwa wakishangaa na kuhoji usajili unaofanyika bila kocha ikiwa ni pamoja na mazoezi yanayoendelea, lakini habari za uhakika ni kwamba tayari kocha mkuu wa kuinoa timu hiyo ameshapatikana na kuanza kazi kwa kutuma programu ambazo zinatumiwa mazoezini na msaidizi wake, Berdien. Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Wakili Simon Patrick, amewataka Wanayanga kutulia huku akiwaeleza kila kitu kinakwenda vizuri ikiwa ni pamoja na kocha huyo kuanza kazi kwa kutuma programu zake ambazo zinatumika mazoezini kwa sasa. Anayetajwa kuwa kocha ni Cedric Kaze kutoka Burundi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako