• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Patashika ya usajili barani Ulaya inazidi kuendelea huku nyota wakubwa wakitafutwa

    (GMT+08:00) 2020-08-20 19:10:52

    Wakati klabu za ulaya zinaendelea kuimarisha vikosi vyao kwa ajili ya msimu ujao, Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane anaendelea kupiga mahesabu ya kumpata mshambuliaji katika dirisha hili la usajili ili kukiongezea nguvu kikosi chake kinachokabiliwa na kazi ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Hispania katik msimu ujao. Baada ya kutolewa na Manchester City katika hatua ya 16 ya Ligi ya Mbingwa Ulaya, Zidane ana kazi moja ya kuhakikisha anatetea ubingwa huo dhidi ya wapinzani wao, Barcelona ambao tayari wameanza kuimarisha kikosi chao kwa kuwa na kocha mpya mholanzi Ronal Koeman. Zidane ameweka wazi kuwa kijana Kylian Mbappe kama chaguo lake namba moja katika usajili huo, akilenga kumuunganisha na mfaransa mwenzake Karim Benzema katika idara ya ushambuliaji. Gareth Bale aliyekuwa chaguo la Zidane anaonekana si sehemu tena ya mipango ya Zidane.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako