• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Bayern yaibuka mabingwa wa UEFA kwa mara ya 6

    (GMT+08:00) 2020-08-24 16:22:14

    Bao la ufundi kupitia kichwa kutoka kwa Kingsley Coman katika kipindi cha pili uwanjani Estadio do Sport Lisboa liliiwezesha Bayern Munich kuifunga Paris Saint-Germain na kushinda taji la Ligi ya Mabingwa kwa mara ya sita. PSG iliifunga RB Leipzig na kuandikisha historia ya kuingia kwenye fainali ya mtanange huo wa Ulaya kwa mara ya kwanza, huku Bayern wakiwaondoa Lyon kupata tiketi hiyo. Mabingwa hao wa Ufaransa walikuwa kwenye harakati ya kuendeleza ubabe wao wakiwa na matumaini ya kubeba taji hilo kwa mara ya kwanza. PSG walipoteza nafasi nyingi za kupata bao la kufutia machozi huku Mbappe akikaribia kutingisha wavu dakika ya lala salama lakini Neuer alikuwa makini kumzuia. Hatimaye Bavarians walishikilia ushindi wao nyerezi na kuibuka washindi mara sita wa mtanange huo wa bara Ulaya na kuvunja rekodi ya Liverpool.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako