• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Sarpong: Nimefurahi kuwa mwanafamilia Young Africans

    (GMT+08:00) 2020-08-25 15:55:41

    Mashabiki wa klabu ya Young Africans wanaamini usajili wa Mshambuliaji kutoka Ghana Michael Sarpong, huenda ukawa jibu sahihi la maswali waliyokua wanajiuliza, nani atakua mbadala wa David Molinga aliyeondoka klabuni hapo siku kadhaa zilizopita. Molinga alikuwa sehemu ya wachezaji walioachwa na uongozi wa Young Africans, kufuatia viwango vyao kutoridhisha msimu uliopita, hatua ambayo ilifungua milango kwa wachezaji wengine kusajiliwa katika kipindi hiki cha kuelekea msimu wa 2020/21. Sarpong ambaye amejiunga na Young Africans, baada ya kuachwa huru na Rayon Sports ya Rwanda, anakuwa mchezaji wa tatu wa kimataifa kusajiliwa na klabu hiyo msimu huu, baada ya viungo wawili raia wa DR Congo, Tusila Kisinda na Mukoko Tunombe waliotua wakitokea AS Vita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako