• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: AK Kufanyia Wanariadha 230 Majaribio Kabla Ya Kuwachuja Kwa Mbio Za Kip Keino Classic Za Oktoba 3

    (GMT+08:00) 2020-08-25 15:59:07

    Shirikisho la Riadha la Kenya (AK) limeteua wanariadha 230 kwa majaribio yatakayofanyika Septemba 12 kabla ya mbio za Kip Keino Classic kuandaliwa ugani Nyayo, Nairobi mnamo Oktoba 3, 2020. Mkurugenzi wa mashindano katika AK, Paul Mutwii, amesema orodha ya watakaoshiriki mbio za Kip Keino Classic ambazo ni za mwisho kwenye msururu wa Riadha wa World Athletics Continental Tour, itatolewa rasmi hii leo. Kwa mujibu wa Mutwii, washiriki waliteuliwa kutokana na ubora wa fomu zao kwa sasa matokeo yao kwenye Riadha za Dunia za 2019 jijini Doha, Qatar na nafasi wanazozishikilia kwenye msimamo wa orodha ya viwango bora vya Shirikisho la Riadha Duniani (IAAF). Fani zitakazoshindaniwa kwenye Mbio za Kip Keino Classic ni kuruka mara tatu, urushaji wa kijiwe, mbio za mita 200, mita 3,000 kuruka viunzi na maji (wanaume na wanawake), urushaji mkuki (wanaume), mbio za mita 400, mita 800, mita 1,500 na mita 5,000 (wanaume na wanawake). Fani nyinginezo ni matembezi ya kilomita 20, kuruka juu (wanaume), kuruka urefu (wanawake), mita 4 x 400 kupokezana vijiti, mita 400 kuruka viunzi na mita 10,000 (wanaume).

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako