• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RAGA: Wakenya watatu, raia mmoja wa kigeni kuhojiwa zaidi katika mchakato wa kupata kocha mpya wa Shujaa

    (GMT+08:00) 2020-08-26 15:53:14

    Dalili zote sasa zinaashiria kwamba kocha mpya wa timu ya taifa ya wanaraga saba kila upande ya nchini Kenya, Shujaa, atakuwa raia wan chi hiyo. Hii ni baada ya Mkurugenzi wa Raga katika Shirikisho la Raga la Kenya (KRU), Thomas Odundo, kusema raia mmoja wa kigeni na Wakenya watatu wamefaulu kuunga orodha fupi ya mwisho ya wakufunzi wanne watakaohojiwa kwa kina zaidi kufikia mwisho wa wiki hii. Mmoja kati ya wanne hao kwenye orodha fupi ya mwisho atapata nafasi ya kurithi mikoba iliyoachwa na Paul Feeney – kocha raia wa New Zealand aliyeagana rasmi na KRU Juni 12, 2020.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako