• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Mashabiki kuruhusiwa uwanjani-mchezo wa Super Cup

    (GMT+08:00) 2020-08-26 15:55:03

    Mashabiki wa Bayern Munich na Sevilla wataruhusiwa kuingia uwanjani kwenye mchezo wa EUFA Super utakaochezwa September 12 katika uwanja wa Puskas Arena huko Budapest, Hungary. Shirikisho la Soka la Ulaya (UEFA) limethibitisha kuwa mashabiki wataruhusiwa kuingia uwanjani kushuhudia mchezo utakaowakutanisha mabingwa wa klabu Bingwa Ulaya UEFA Bayern Munich ya Ujerumani dhidi ya mabingwa wa michuano ya UEFA Europe League Sevilla ya Hispania. Ni asilimia 30% tu ya mashabiki, sawa na mashabiki 20,000 tu ndio watakaoruhusiwa kuingia uwanjani, ingawa uwanja huo una uwezo wa kuchuka mashabiki 680000. Uamuzi huo umechukuliwa ikiwa ni njia ya kuzuia kuenea kwa maambukizi ya virusi vya Corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako