• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Azam FC Waboresha mikataba benchi la ufundi

    (GMT+08:00) 2020-08-26 15:57:42

    Klabu ya Azam FC imewaongezea mkataba makocha wake watatu wanaounda benchi la ufundi, kwa ajili ya kuendelea kuwa ndani ya kikosi hicho kwa msimu wa 2020/21. Kocha Mkuu Aristica Cioaba kutoka Romania amekamilisha mpango huo sanjari na wasaidizi wake Bahati Vivier wa Burundi na Kocha wa Viungo, Costel Birsan. Taarifa kutoka Azam FC zimeeleza kuwa, makocha hao wamesaini mkataba wa mwaka mmoja kila mmoja. Mwishoni mwa juma lililopita Azam FC waliwatambulisha wachezaji wao wapya pamoja na benchi la ufundi ambalo lilianza kazi kwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Namung FC, katika Uwanja wa Azam Complex.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako