• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Rais wa Barcelona akataa kujiuzulu kisa Messi kuondoka

    (GMT+08:00) 2020-08-27 16:11:02

    Rais wa klabu ya Barcelona Josep Maria Bartomeu amepinga mtizamo wa mashabiki wa timu hiyo wanaomtaka ajiuzulu endapo Lionel Messi ataondoka. Lionel Messi aliwasilisha maombi rasmi kwa Uongozi wa Timu ya Barcelona akitaka kuondoka katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya kiangazi, suala lililoleta taharuki kubwa kwa wanachama na mashabiki wa timu hiyo duniani kote. Bartomeu anatuhumiwa kuzembea hadi Messi kuchukua hatua hii, japo ukweli ni kuwa kichapo cha bao 8-2 dhidi ya Bayern Munich katika hatua ya nusu fainali ya Mabingwa Barani Ulaya ndio iliyosababisha haya yote huku kocha Quique Setien na Mkurugenzi wa ufundi Eric Abidal wakifukuzwa kazi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako