• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Magharibi B yatoa zawadi kwa washindi

    (GMT+08:00) 2020-08-27 16:11:47

    UONGOZI wa Soka Wilaya ya Maghabibi 'B' Unguja umekabidhi zawadi kwa timu zilizopata ubingwa na kupanda daraja la pili kwenda Mkoa na la tatu kwenda la pili Wilaya. Akizungumza mara ya kukabidhi zawadi hizo huko uwanja wa michezo Maungani Katibu wa Soka Wilaya hiyo Omar Abuu alisema, licha ya kuwa na zawadi kidogo,lakini anaamini kuwa zitawasaidia. Alisema lengo lao kutoa zawadi nyingi ambazo zingesaidia kwenye usajili wao,lakini kutokana na hali walilazimika kutoa walichokipata. Alizitaka timu ambazo zimepata nafasi ya kupanda daraja msimu huu, kujiandaa vyema kwa ajili ya kupambana,huku daraja walilopanda ni gumu zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako