• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: Victor 'Rabbit' Chumo Kumwekea Kasi Kipchoge Katika Mbio Za London Marathon

    (GMT+08:00) 2020-08-27 16:12:24

    Bingwa wa mbio za Barcelona Half Marathon, Victor 'Rabbit' Chumo, atakuwa miongoni mwa wanariadha watakaoweka kasi kwenye kivumbi cha London Marathon, Uingereza mnamo Oktoba 4. Chumo atatoa upinzani kwa Eliud Kipchoge ambaye ni mshikilizi wa rekodi ya dunia kwenye mbio hizo za kilomita 42. Chumo alikuwa pia katika kundi la wanariadha waliomtia kasi Kipchoge wakati alipoweka historia ya kuwa mwanadamu wa kwanza kuwahi kukamilisha mbio za kilomita 42 chini ya saa mbili. Bingwa mara nne wa dunia na Olimpiki katika mbio za mita 5,000 na mita 10,000 Mo Farah, naye atawatoa jasho Waingereza Matt Clowes na Jake Smith wanaopania kutumia London Marathon kusajili muda wa kufuzu kwa Olimpiki za Tokyo, Japan mwakani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako