• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wakulima wa zabibu Tanzania waomba kukatiwa bima

  (GMT+08:00) 2020-08-27 19:27:27
  Wakulima wa zao la zabibu mkoani Dodoma, wanaomba kukatiwa bila zitakazowalinda wkaati wa majanga.

  Baadhi ya wakulima waliopo kijiji cha Matumbulu,nje kidogo ya jiji la Dodoma wameiomba serikali na taasisi za kifedha zinazotoa huduma za bima kuwakatia bima ili ziwasaidie wakati wa majanga.

  Wakulima hao wansema sababu ya kuhitaji bima za kilimo ni kutokana na wengi wao kukosa mazao kwenye msimu huu kwa sababu ya mvua kubwa.

  Wakulima hao wanasema zao hilo halihitaji maji mengi ,hivyo ikitokea mvua zikizidi kama msimu huu inakuwa ni changamoto kwao kupata mazao ya kutosha.

  Aidha wakulima hao wanasema katika msimu huu wengi wao wamekosa mazao kutokana na mvua nyingi zilizonyesha na kusababisha mavuno kidogo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako