• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Golikipa wa Harambee Stars asakwa na timu za ndani na nje ya Kenya

    (GMT+08:00) 2020-08-28 17:11:05

    Licha ya kutoshiriki mchuano wowote tangu Novemba 2019 golikipa matata wa timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars, John Oyemba, amethibitisha kwamba huduma zake zinawaniwa na vikosi saba tofauti ndani na nje ya nchi. Mlindamlango huyo alipata jeraha baya la mgongo mwaka 2019 na akasalia bila klabu kuanzia Januari 2020 baada ya mkataba wake na Kariobangi Sharks kumalizika. Hata hivyo, wingu la matumaini limeanza kumshukia golikipa huyo ambaye kwa sasa anafukiziwa na klabu tano za nchini Kenya na mbili za nje. Timu za Tusker, AFC Leopards, Posta Rangers, Nairobi City Stars na Bidco United ni kati ya timu za Ligi Kuu ya Kenya ambazo zimeweka wazi nia ya kupata saini ya Oyemba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako