• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Pogba akutwa na virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-08-28 17:11:21

    Kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa Didier Deschamps amesema, kiungo mahiri wa timu ya Manchester United, Paul Pogba, amekutwa na virusi vya Corona, na kwamba mchezaji huyo kwa sasa amejitenga kwa siku 14. Hatua hiyo inamfanya Pogba kukosa mechi ya timu ya taifa ya Ufaransa katika Ligi ya Mataifa ya UEFA dhidi ya Sweden itakayochezwa Septemba 5 ugenini na mechi nyingine dhidi ya Croatia itakayochezwa jijini Paris siku tatu baadaye. Hata hivyo, Pogba atakuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kuichezeka klabu yake ya Manchester United watakapofungua rasmi kampeni zao za Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) msimu huu wa 2020-21 dhidi ya Crystal Palace. Mechi hiyo itachezewa uwanjani Old Trafford Septemba 19.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako