• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wakenya 28,000 Kupokea Msaada Wa Chakula Kutoka kwa kampuni ya Base Titanium

  (GMT+08:00) 2020-08-28 18:44:03

  Zaidi ya familia 28,000 zisizojiweza kutoka eneo la Kinango, Kaunti ya Kwale zimepangiwa kupokea chakula cha msaada kutoka kwa serikali ya kaunti hiyo na kampuni ya kuchimba madini ya Base Titanium.

  Kulingana na gavana wa kaunti hiyo Salim Mvurya, familia nyingi katika eneo hilo zinakumbwa na uhaba wa chakula kufuatia mazao yao kukosa kufanya vizuri.

  Miongoni mwa vitu watakavyopatiwa ni unga wa ngano, unga wa mahindi, maharagwe, chumvi, na mafuta ya kupikia. Vile vile watapokea sanitaiza na maski.

  Serikali ya Kaunti ya Kwale imesema wamekuwa wakishirikiana na washikadau mbalimbali kuwasaidia wakazi wa kaunti hiyo kupata bidhaa muhimu kujikimu kimaisha. Maisha ya wengi yameathirika kufuatia janga la corona.

  Wengi wa wakazi wa kaunti hiyo walitegemea sekta ya utalii lakini sekta hiyo ilidorora baada ya kuzuka janga la corona. Wakazi wengi walipoteza ajira.

  Aidha serikali ya kaunti imewatahadharisha wakazi dhidi ya kupuuza masharti yaliyowekwa kudhibiti ugonjwa wa Covid-19.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako