• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • BENKI YA EQUITY YAPATA MWENYEKITI MPYA

  (GMT+08:00) 2020-08-31 15:49:15

  Benki ya Equity imemteua balozi Erastus Mwencha awe mwenyekiti mpya wa bodi yake.

  Bw Mwencha alichukua wadhifa huo mwishoninmwa wiki jana, kutoka kwa Prof Isaac Macharia ambaye alipandishwa cheo na kuteuliwa mwenyekiti wa bodi ya Kampuni ya Equity Holdings.

  Akizungumza baada ya kupokezwa wadhifa huo, Bw Mwencha aliahidi kukuza benki hiyo kiuchumi na pia kuboresha mazingira yake kibiashara na jinsi inavyowahudumia wateja wake.

  Anachukuwa nafasi hiyo wakati ambapo sekta ya benki ikiwa miongoni mwa sekta zilizoathirika vibaya na janga la virusi vya corona nchini Kenya. Hata hivyo, bwana Mwecha ameahidi kuhakikisha kwamba benki hiyo itaendelea kupanua matawi yake na kutumia nafasi iliyopo kwenye miungano ya kibiashara kama COMESA na EACC kupenya katika masoko ya nje. Balozi huyo ana tajriba mkubwa katika usimamizi wa bodi za kampuni mbalimbali.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako