• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WAGENI WANAOWASILI KENYA KUTOKA MATAIFA AMBAYO KENYA INAYAONA KUWA HATARI KWA VIRUSI VYA CORONA, WATAWEKWA KARANTINI YA SIKU 14

    (GMT+08:00) 2020-08-31 15:49:40

    Waziri wa Utalii na Wanyamapori wa Kenya, Najib Balala, amesisitiza kwamba raia wa nchi ambazo Kenya inaziona ziko katika hatari ya maambukizi ya corona, watawekwa karantini ya lazima wanapowasili humu nchini.

    Waziri Balala alisema raia hao watawekwa karantini ya lazima ya siku 14 kulingana na mwongozo wa Shirika la Afya Duniani. Waziri huyo alisema Kenya itaendelea kudumisha usalama wa watalii katika juhudi za kuimarisha sekta ya utalii.

    Wakati huo huo, Bw Balala alisema nchi za Kenya na Tanzania zinaendelea na mazungumzo kabambe ili kuanzisha usafiri wa ndege zao za kitaifa za Kenya Airways na Precision Air ili ziwe zinakubalika kutua na kupaa katika anga ya kila mojawapo ya mataifa haya mawili.

    Nchi hizo zimekuwa kwenye mgogoro ambao kwa kiasi kikubwa unahusu janga la virusi vya corona.

    Tanzania imekuwa ikisisitiza inakabiliana na janga hilo jinsi inavyostahili. Bw Balala alisema mipaka ya Kenya ingali imefungwa lakini watalii wanaoingia humu nchini kupitia viwanja vya kimataifa vya ndege ni sharti wafuate kanuni za afya ili kudhibiti maambukizi ya virusi hivyo. Balala aliyasema haya alipokuwa akizungumza na wawekezaji katika sekta ya utalii nchini Kenya.

    Mwekezaji mmoja aliuliza endapo watanzania wanaruhusiwa kuingia nchi ya Kenya kupitia mpaka wa Namanga, hata hivyo waziri huyo alisisitiza kuwa Kenya ingali imefunga mipaka yake. Kwenye mkutano huo wa wawekezaji wa utalii kutoka nchi za Kenya, Rwanda, Tanzania miongoni mwa zengine walijadili namna ya kuimarisha sekta hiyo wakati wanapokabiliana na janga hilo.

    Hata hivyo, mkurugenzi mkuu wa Bodi ya Utalii nchini Tanzania Devota Mdachi alisema nchi yake haina haja ya kuweka wageni kwenye karantini bora wawe na sakabadhi halali za kuonyesha walipimwa na hawana virusi hivyo.

    Bi Mdachi alisema Mei 2020 mbuga ya kitaifa ya wanyama wa porini ya Serengeti ilipokea wageni 20 wa kitaifa lakini Julai zaidi ya watalii 270 walimiminika katika sehemu hiyo kuangalia nyumbu wakivuka kutokea mbuga ya Maasai Mara nchini Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako