• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Simba yatwaa ubingwa wa Ngao ya Jamii baada ya kuirarua Namungo Fc 2-0

    (GMT+08:00) 2020-08-31 16:12:40

    Klabu ya Simba ilifanikiwa kutwaa Ubingwa wa Ngao ya Jamii baada ya hapo jana kuifunga Namungo Fc bao mbili kwa sifuri katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha na kuweka rekodi mbali mbali. Ushindi katika mchezo huo umewafanya wekundu wa msimbazi kuandika historia ya kutwaa taji la michuano hiyo mara nyingi zaidi ikiwa imefanya mara sita. Simba Sc kabla ya jana ilichukua taji hilo mwaka 2011, 2012,2017, 2018 na 2019 sawa na watani wao Yanga ambao wenyewe walichukua mwaka 2001, 2010, 2013, 2014 na 2015. Mabao ya Simba yaliyofungwa na Nahodha wake John Bocco kwa penati na Benard Morrison. Kwa upande wa Namungo, iwapo wangepata ushindi ingekua timu ya kwanza kutoka Kanda ya Kusini ambayo ilishiriki ligi kwa msimu mmoja tu Ligi Kuu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako