• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Arsenali yainyuka Liverpool 5-4 na kuchukua kombe la Shield

    (GMT+08:00) 2020-08-31 16:13:03

    Arsenali wanaendelea kusherekea ushindi baada ya kuinyuka Liverpool mabao 5-4 na kuchukua kombe la Shield. Kwenye mechi hiyo iliyokuwa ikisakatwa ugani Wembley awali walitoka sare ya 1-1 ndani ya dakika 120 na kulazimu penati. Arsenal ndio walikuwa wa kwanza kuona lango kwenye dakika ya 12 baada ya nahodha Emerick Aubameyang kucheka na wavu. The reds hata hivyo walijikakamua na kusawazisha bao hilo dakika ya 73 na hapo mambo yakawa ni kila mmoja kulinda chake. Aubameyang ndiye pia aliipa Arsenal penati ya ushindi baada ya kiungo wa Liverpool Rhian Brewster kutema shoti yake nje. Liverpool itawalazimu kutafuta huduma za mganga kujua tatizo lao kwani mwaka jana pia walipoteza penati walipokutana na Manchester City kwenye kombe hilo. Kocha wa Arsenal Mikel Arteta amesema ombi lake kwa sasa ni kutompoteza Aubameyang na akubali kutia upya saini mkataba wake. Mabao yake 71 katika mechi 110 alizocheza zimeifanya timu hiyo kunyakua tuzo mbili ndani ya mwezi mmoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako