• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Yanga SC yaibanjua Aigle Noir 2-0 katika mchezo wa kirafiki wa Wiki ya Mwananchi

    (GMT+08:00) 2020-08-31 16:13:22

    Vigogo wa soka Tanzania, Yanga SC usiku wa jana waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya mabingwa wa Burundi, Aigle Noir katika mchezo wa kirafiki uliopigwa uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi. Katika mchezo huo uliohudhuriwa na Rais mstaafu wa awamu ya Nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, Aigle Noir iliwaruhusu Yanga kupata mabao baada ya kiungo wake, Mghana Koffi Kouassi kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 29 kufuatia kuonyeshwa kadi ya njano ya pili na refa Martin Saanya wa Morogoro. Baada ya hapo Yanga SC wakapata bao la kwanza dakika ya 39 likifungwa na winga wake mpya, Tuisila Kisinda aliyemchambua kipa Mtanzania wa Aigle Noir, Erick Johola kufuatia pasi nzuri ya Feisal. Mshambulaji mpya, Mghana Michael Sarpong akaifungia Yanga SC bao la pili dakika ya 59 kwa kichwa kikali kutoka umbali wa mita sita kufuatia krosi maridhawa ya Ditram Nchimbi. Na ikashuhudiwa kipindi cha pili kocha mpya wa Yanga SC, Mserbia Zlatko Krmpotic akibadili kikosi kizima.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako