• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Kocha msaidizi wa Yanga asema wanahitaji muda tu kukijenga kikosi cha ushindani

    (GMT+08:00) 2020-09-01 18:13:52

    Kocha msaidizi wa Klabu ya Yanga, Juma Mwambusi amesema wanahitaji muda kukijenga kikosi cha ushindani katika msimu wa mashindano unaotarajiwa kuanza septemba tisa mwaka huu. Mwambusi ambaye aliwahi kuifundisha miamba hiyo ya soka akiwa na Makocha Hans Van Pluijm na George Lwandamina kwa nyakati tofauti, alirejeshwa hivi karibuni na sasa ndiye msaidizi wa mserbia Zlatko Krmpotik ambaye aliwasili siku ya Ijumaa. Yanga itafungua dimba kwa kumenyana na Tanzania Prisons mchezo utakaopigwa tarehe saba ya mwezi huu siku ya Jumapili katika uwanja wa Mkapa Jijini Dar es salaam.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako