• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Yanga yalaani kitendo cha mashabiki wake kumfanyia fujo shabiki wa Simba, Mo Dewji asema ataka kukutana na shabiki huyo

    (GMT+08:00) 2020-09-01 18:14:22

    Klabu ya Yanga SC ya Dar es Salaam imelaani vikali kitendo cha mashabiki wake, kumfanyia fujo shabiki wa timu pinzani, Simba SC. Mashabiki hao walimpiga na kumchania nguo shabiki aliyekuwa amevalia jezi ya Simba. Yanga imekasirishwa na kusema haiungi mkono vitendo vinavyoashiria kuvunja amani na kuondoa uungwana michezoni.

    Wakati huohuo mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Mohamed Dewji anamsaka shabiki wa Simba aliyechaniwa jezi yake kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi na video kusambaa mitandaoni. Kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter Mo Dewji ameweka video ya shabiki huyo na kuandika ujumbe mpira ni ushindani sio uadui, na kwamba anamtafuta shabiki huyu wa Simba kwani anataka kukutana nae. Tukio la kuchaniwa jezi na kuzongwa na mashabiki hao limezua mijadala mitandaoni watu wakilaani kitendo hicho ambacho sio cha kiungwana michezoni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako