• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • CAF yazipiga chini Yanga, Azam

    (GMT+08:00) 2020-09-02 16:31:22

    Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) hatimaye limemaliza kitendawili cha timu zitakazowakilisha Tanzania kwenye Klabu Bingwa Afrika na Kombe la Shirikisho 2020/21. Yanga na Azam ziliweka matumaini ya kushiriki michuano hiyo baada ya Libya kuahirisha ligi yao na Tanzania iliyokuwa na alama 14 ilikuwa na nafasi ya kupenya endapo Libya wangepigwa chini na CAF. Taarifa rasmi iliyotolewa na CAF jana Septemba Mosi, 2020 imezitaja nchi 12 zenye pointi nyingi ambazo zitatoa timu nne kwenye michuano ya Bara la Afrika ikiwemo Libya ambayo haikumaliza msimu wake wa Ligi Kuu 2019/20. Usajili wa timu hizo kwa nchi wanachama umeanza Septemba Mosi yaani jana hadi Oktoba 20 na kutokana na janga la corona Ligi nyingi zilisimama CAF wametoa ufafanuzi suala hilo. CAF imesema nchi ambazo hazikumaliza ligi na zilitoa taarifa awali zinaruhusiwa kushiriki kwa mujibu wa msimamo wa Ligi wa nchi husika na pointi. Pia imeeleza kwa nchi ambazo ziliahirisha ligi yao timu zitaendelea na uwakilishi kwenye michuano hiyo kulinga na uwiano utaotolewa na shirikisho la nchi husika. CAF wamesema kwa nchi ambazo hazijamaliza ligi zao wana haki ya kuchagua njia mbili walizoainisha kabla ya kufungwa kwa dirisha. Ratiba ya mtoano itaanza kwa raundi ya kwanza Novemba 20-22 na kurudiana Novemba 27-29 huku hatua ya ya kwanza ikianza Disemba 11-13 na kurudiana 18-20. Dirisha la usajili litafunguliwa Oktoba 21 hadi Novemba 5 na litafunguliwa tena Novemba 6 hadi 19.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako