• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Manara atolea ufafanuzi taarifa za Meddie Kagere kupigana na Kocha Sven Vandenbroeck

    (GMT+08:00) 2020-09-02 16:31:45

    Uongozi wa simba umesema kuwa taarifa zinazoenea mitandaoni na kwenye baadhi ya vyombo vya habari zikieleza kuwa mchezaji wao nyota Meddie Kagere amepigana na Kocha Mkuu Sven Vandenbroeck sio za kweli. Ofisa Habari wa Simba Haji Manara amesema kuwa kumekuwa na taarifa ambazo zinasambaa kwenye mitandao ya kijamii zikieleza kuwa Kagere na Sven wamepigana jambo ambalo ni la kupikwa.

    "Kwetu sisi Simba ni furaha siku zote na mambo hayo yalikuwa kitambo sio sasa kila kitu kinakwenda sawa hakuna ukweli wowote kuhusu Kagere kupigana na Sven.

    "Huo ni uogo na umepikwa kusudi na kwa nia ovu ya kutuvuruga kwa kuwa mambo ndani ya Simba ni shwari hivyo tumeshajua na hatupo tayari kuvurugwa.

    Simba ipo Mbeya ambapo iliwasili jana Septemba Mosi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa Septemba 6, Uwanja wa Sokoine dhidi ya Ihefu FC.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako