• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: LaLiga yaamua kuweka wazi swala la Messi

    (GMT+08:00) 2020-09-02 16:32:02

    Shirikisho la soka nchini Hispania, LaLiga limesema kuwa limefuatilia kwa karibu taarifa zilizokuwa zikiripotiwa na vyombo mbalimbali vya Habari kuhusu Mkataba wa mchezaji, Lionel Andres Messi na klabu ya FC Barcelona na baada ya kuupitia mkataba huo, LaLiga imeona ipo haja ya kufafanua juu ya swala hilo. Mkataba unaotumika sasa una kipengele cha 'release clause' ambacho kitatumika kama, Lionel Andres Messi ataamua kukatisha mkataba wake mapema kwa mujibu wa kifungu cha 16, amri ya Kifalme (Royal Decree 1006/1985 ya Juni 26) kwa sheria za Hispania ambayo ndiyo husimamia kazi za taaluma ya wanamichezo. Sambamba na kanuni na utaratibu unaotumika katika matukio kama hayo, LaLiga haitaendelea na kutolewa kwa mchezaji anayehitajika kufutiwa usajili kutoka kwa Shirikisho la Soka la Uhispania isipokuwa kifungu kilichotajwa hapo awali kimeshalipwa. Hivyo 'release clause' bado inafanya kazi ni tofauti na yeye Messi anavyoamini kuwa anaweza kuondoka pasipo na hiyo kutokana na sehemu ya mkataba wake kuwepo makubaliano yanayomruhusu kuondoka kama atahitaji kufanya hivyo kila ifikapo mwisho wa msimu. Inaelezwa kuwa Lionel Messi Jumapili hii hakwenda kufanyiwa vipimo vya Corona ndani ya Barcelona ili kuwa tayari kwa maandalizi ya msimu mpya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako