Ndege ya Kitaifa imesema hatua hiyo inakusudiwa kuwaheshimu wafanyikazi wa afya walio katika mstari wa mbele kupamabana na janga la Corona , ambalo hadi kufikia sasa limeua watu 572, na 19,590 wamepona.
Katika taarifa, KQ imesema wafanyikazi wa afya watatakiwa kuonyesha Kadi yao ya kitambulisho wakati wa ununuzi wa tiketi.
Ofa hii ni ya mwezi mmoja na ilianza jana, na wafanyikazi wa afya sasa watasafiri kwa nauli ilipunguzwa kwa asilimia 50.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |