• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TENISI: Djokovic aendeleza kipigo kwa kumshinda Kyle Edmund na kufuzu raundi ya tatu ya michuano ya wazi ya Marekani

    (GMT+08:00) 2020-09-03 18:38:19

    Nyota namba moja kwenye mchezo wa Tenis Duniani kwa Wanaume, Novak Djokovic ameendeleza rekodi ya kutopoteza mchezo tangu kuanza kwa mwaka 2020 baada ya kumshinda Kyle Edmund na kufuzu raundi ya tatu ya michuano ya wazi ya Marekani. Djokovic alishinda kwa seti 6-7,(5-7),6-3,6-4,6-2, na kumuondosha Muingereza Kylie Edmund na sasa atacheza dhidi ya Jann-Lennard katika raundi ya tatu akiwa na lengo la kutwaa Grand Slam yake ya 18. Kwa upande wa nyota mwingine Norrie Cameroon alitinga raundi ya tatu ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza baada ya kumshinda Federico Coria kwa seti 6-3,6-4,6-4. Mshindani wa Djokovic katika michuano hii ni Muingereza Andy Murray ambaye na yeye anashiriki michuano ya Grand Slam kwa mara ya kwanza baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu akiwa anauguza majeraha ya nyonga lakini wababe kama Roger Federer na Rafael Nadal wote hawapo mashindanoni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako