• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Mikel Arteta asema Aubameyang bado yupo sana Arsenal

    (GMT+08:00) 2020-09-03 18:39:12

    Kocha Mkuu wa Arsenal Mikel Arteta, amesema kuwa mshambuliaji wake namba moja Pierre Emerick Aubameyang atasaini dili jipya hivi karibuni. Arteta ameongoza kikosi chake kutwaa mataji mawili kwa kuzinyoosha timu kubwa ikiwa ni pamoja na lile la Kombe la FA ambapo aliichapa Chelsea mabao 2-1 na taji la Ngao ya Jamii alishinda kwa penalti 5-4 mbele ya Liverpool baada ya dakika 90 kutoka sare ya bao 1-1. Mtupiaji wa mabao yote matatu alikuwa ni nahodha Aubameyang ambaye amekuwa akitajwa kutaka kuondoka ndani ya kikosi hicho. Msimu mpya wa Ligi Kuu England unatarajiwa kuanza Septemba 12 na mabingwa watetezi ni Liverpool.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako