• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • CORONA: PSG yapata pigo watatu wana corona akiwemo Neymar

    (GMT+08:00) 2020-09-03 18:40:36

    Klabu ya soka ya Ufaransa PSG imethibitisha kupitia Twitter kuwa wachezaji wake watatu wana ugonjwa wa Covid-19. Ingawa haijathibitishwa majina ya wachezaji hao ni Ángel Di María, Leandro Paredes na Neymar. Ili kuzuia maambukizi zaidi ya virusi vya corona miongoni mwa wachezaji, klabu hiyo imechukua hatua za kuwaweka karantini wachezaji hao. Kufuatia kupigwa 1-0 kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa na Bayern Munich, PSG iliiomba Ligi ya Ufaransa kuahirisha mechi yake ya pili pia kutoka Jumamosi, Agosti 29 saa 21:00 hadi Alhamisi, Oktoba 10. PSG ilisema sababu ya ombi hilo ni kuwapa wachezaji nafasi ya kupumzika baada ya kucheza mechi tatu katika kipindi cha siku 10, Ligi ya Mabingwa, hata hivyo, wachezaji, wakiwamo Neymar, Di María na Paredes waliamua kuzidisha likizo yao jijini Ibiza, ambako wanadaiwa kunaswa na virusi vya Covid-19.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako