• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya-Hali ngumu ya maisha yasababisha idadi ya watu katika kivuko cha Likoni,Mombasa kupungua maradufu

  (GMT+08:00) 2020-09-03 19:38:25
  Idadi ya watu wanaotumia kivuko cha Likoni,mjini Mombasa,nchini Kenya,imepungua maradufu tangu janga la corona lilipoanza kuenea mjini humo.

  Haya ni kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Shirika la Huduma za Feri nchini Kenya,Bakari Gowa,ambaye amesema idadi ya abiria kivukoni Likoni imepungua kwa kiasi kikubwa na msongamano unaoshuhudiwa ni wa wale wanaokwenda kusaka tonge.

  Alisema wanawake na watoto wanaovuka kivukoni hapo wanaenda kupokea chakula cha msaada kinachotolewa na kampuni ya kutengeza simiti.

  Aliongeza kuwa hali ngumu ya maisha imesababisha kuongezeka kwa idadi ya watu wanaoenda kupokea chakula hicho.

  Gowa anasema msongamano mkubwa wa watu ulitokana na wenyeji wa Likoni waanoenda kutafuta vibarua kila siku lakini tangu kuzuka kwa janga la corona watu wengi walipoteza ajira kufuatia baadhi ya viwanda kufungwa,ndiposa kusababisha idadi ya watu kivukoni hapo kupungua maradufu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako