• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KIKAPU: Houston Rockets yaifunga Oklahoma City Thunder na kufuzu nusu fainali ya NBA

    (GMT+08:00) 2020-09-04 18:35:45

    Timu ya Houston Rockets imefuzu kucheza nusu fainali ya ligi ya mpira wa kikapu nchini Marekani NBA kwa kuifunga Oklahoma City Thunder kwenye mchezo wa mtoano kwa ushindi wa jumla wa mechi 4-3. Rockets walishinda michezo miwili mfululizo ya kwanza lakini OKC walisawazisha hadi kufikia 2-2 wakichagizwa na kiwango bora cha staa wao Chris Paul. Kurejea kwa Russell Westbrook ambaye alikua nje kwa majeraha kulirejesha makali ya Houston Rockets, aliwasaidia kuwarejesha mchezoni na kushinda mchezo wa tatu, kabla ya alfajiri ya jana kumaliza kazi kwa kushinda kwa alama 104-102. Russell Westbrook ameonekana kuibeba zaidi Houston Rockets katika michezo miwili ya mwanzo ambayo walishinda lakini alipopata majeraha walifungwa michezo miwili mfululizo. Uwepo wa Westbrook pia ulipelekea kushusha alama za staa wa OKC, Chris Paul ambaye siku zote amekua akifunga alama zaidi ya 25 tangu kuanza kwa hatua ya mtoano. Licha ya Oklahoma City Thunder kupoteza, Chris Paul amefanya Triple Double akiwa amefunga points 19, assists 12, rebound 11. Houston Rockets sasa watakabiliana na Los Angeles Lakers katika mchezo wa nusu fainali ya ukanda wa Magharibi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako