• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: Kutoandaliwa kwa mbio za nyika kwasababisha Wakenya wapunguze kasi yao

    (GMT+08:00) 2020-09-04 18:36:28

    Kutoandaliwa kwa mbio zozote za nyika hadi kufikia sasa kumechangia matokeo mseto yaliyosajiliwa na Wakenya kwenye duru mbili za ufunguzi wa kivumbi cha Wanda Diamond League. Haya ni kwa mujibu wa kocha wa timu ya taifa ya riadha, Julius Kirwa ambaye ameshikilia kwamba mbio za nyika zimekuwa zikiwapa wanariadha wa Kenya jukwaa mwafaka la kujiandaa kwa mashindano mbalimbali ya kimataifa kila msimu. Kilele cha msimu wa mbio za nyika mwaka huu kingekuwa kiandaliwe kwa kivumbi cha Afrika nchini Togo mnamo Aprili. Hata hivyo, janga la corona lilichangia kuahirishwa kwa mbio hizo mnamo Machi. Ingawa hivyo, Kirwa anaamini kwamba matokeo ya Wakenya yataimarika zaidi katika duru zilizosalia za Brussels, Ubelgiji (Septemba 4), Naples, Italia (Septemba 17), Doha, Qatar (Septemba 25) na China (Oktoba 17). Wakati uo huo, bingwa wa Olimpiki katika mbio za mita 1,500, Faith Chepng'etich amesema atajaribu kuvunja rekodi ya mbio za mita 1,000 kwenye kivumbi cha Diamond League kitakachoandaliwa ugani AG Memorial Van Damme jijini Brussels leo Ijumaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako