• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Kimejulikana sasa Messi bado ataendelea kuwepo Barcelona

    (GMT+08:00) 2020-09-04 18:36:58

    Mambo yenda yakageuka. Baada ya uvumi wa muda mrefu kwamba Lionel Messi atalazimisha kuondoka Barcelona katika dirisha hili la uhamisho, imebainika kwamba staa huyo anafikiria kubaki Nou Camp. Hatma ya staa huyo imezua maswali baada ya kuripotiwa kuuandikia uongozi barua kuufahamisha kuwa anataka kuondoka. Baba wa staa huyo, Jorge Messi, ambaye pia ndiye wakala wake, alikaririwa mapema akisema kwamba ni ngumu kwa mwanawe kuchezea Barca tena na akatua Nou Camp kwa ajili ya kuzungumzia hatima ya Messi. Lakini baada ya "kikao kizito" na mabosi wa klabu hiyo jana, mzee Messi amesema mwanawe atabaki kumalizia mkataba wake. Taarifa za jana zilikuwa ni habari njema kwa klabu ya Barcelona, mashabiki wao na Ligi Kuu ya Hispania ambayo inajaribu kuwavutia watazamaji katika soko la dunia huku ikiwa tayari ilishakimbiwa na mastaa Cristiano Ronaldo aliyeenda Italia na Neymar aliyeenda Ufaransa. Messi alilizua baada ya Barcelona kutolewa kwa mara ya tatu mfululizo katika Ligi ya Mabingwa Ulaya huku mara hii ikiwa ni kwa kipigo cha aibu cha mabao 8-2 kutoka kwa Bayern Munich. Rais wa Barcelona, Bartomeu, pia alidaiwa kumchefua Messi baada ya kuvuja kwa taarifa kwamba amezilipa media binafsi kwa ajili ya kumchafua mshindi huyo mara sita wa tuzo ya Ballon d'Or, tena kwa kutumia pesa za klabu. Na inaaminika kwamba Messi hajafurahishwa na usajili wa baadhi ya nyota wa klabu hiyo katika siku za karibuni ambao wanaonekana hawana sapoti ya kutosha jambo linalomfanya abaki kubeba mzigo mzito wa kuifungia mabao timu na kuwapikia wengine mabao. Msimu uliopita pekee, Messi amefunga mabao 25 na kutoa asisti 21 kwenye mechi 33 za Ligi Kuu ya Hispania alizocheza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako