• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Simba ya Tanzania yaanza vizuri kutetea ubingwa wake, yanga yabanwa mbavu

    (GMT+08:00) 2020-09-07 16:54:38

    Mabingwa watetezi, Simba SC wameuanza vyema msimu mpya wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ihefu SC iliyopanda daraja katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Nahodha na mshambuliaji John Bocco alianza kuwafungia Wekundu wa Msimbazi dakika ya 11 akimalizia pasi nzuri ya kiungo Mghana, Bernard Morrison. Mchezaji wa zamani wa Ndanda FC ya Mtwara, Omary Mponda akaifungia Ihefu SC bao la kusawazisha dakika ya 15 akimalizia pasi ya Willy Mgaya. Muzamil Yassin akaifungia Simba SC bao la ushindi dakika ya 43 akimalizia pasi ya kiungo mwenzake, Mzambia Clatous Chotta Chama. Katika mechi nyingine ya wikiendi iliyopita klabu ya Yanga SC imelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Tanzania Prisons ya Mbeya katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Tanzania Prisons walikuwa wa kwanza kupata goli katika dakika ya saba, mfungaji Lambert Sibiyanka akimalizia pasi ya Jeremiah Juma. Mshambuliaji mpya, Mghana Michael Sarpong akaisawazishia Yanga SC dakika ya 19 baada ya kutokea tafrani kwenye lango la Tanzania Prisons.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako