• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Caster Semenya hatarini kukosa michezo ya Olimpiki ya Tokyo kufuatia uamuzi wa mahakama

    (GMT+08:00) 2020-09-09 17:29:03

    Bingwa mara mbili wa Olimpiki mita 800 Caster Semenya wa Afrika Kusini anaonekana kushindwa kwenye vita yake ya kisheria ya muda mrefu dhidi ya kanuni zinazohitaji wanawake wenye testosterone ya kiwango cha juu kutumia dawa ili kupunguza kiwango hicho, ili waweze kushiriki kwenye mbio za meta 400 hadi maili moja. Mahakama ya Uswisi imesema inaunga mkono uamuzi wa mahakama ya usuluhishi wa michezo uliotolewa mwaka jana kwamba sera na uwanja wa wanariadha walio na tofauti katika ukuaji wa kijinsia (DSD) ilikuwa "muhimu, ya busara na sawia" kuhakikisha ushindani mzuri kwa wanawake michezoni. Kutokana na uamuzi huo inaonekana kuwa bingwa huyo wa medali ya dhahabu kwenye michezo ya Olimpiki ya London 2012 na Rio 2016, hawezi kutetea taji lake huko Tokyo. Caster Semenya alionekana kuwa hana mpinzani kwenye mbio za mita 400 na 800 kutokana na uwezo wake kuwa zaidi ya wanawake anaoshindana naye, na baadhi ya watu kusema huo si ushindani wa haki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako