• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ligi ya mataifa ya Ulaya iliendelea tena jana, Ufaransa, Ureno na Ubelgiji zashinda

    (GMT+08:00) 2020-09-09 17:29:28

    Ligi ya mataifa ya Ulaya iliendelea tena jana katika viwanja mbalimbali, huku Uingereza ikiendelea kutia wasiwasi baada kubanwa mbavu na Denmark mjini Copenhagen kwa kutoka sare ya bila kufungana. Kocha wa England anatakiwa kujiangalia maana ushindi wa bahati dhidi ya ICELAND na sare ya Denmark vitawachanganya wapenzi wa soka Uingereza na kuhitaji matokeo mazuri zaidiā€¦. Ubelgiji wameendelea kupata ushindi kwenye kundi lao baada ya kufanikiwa kuzichapa ICELAND. Ufaransa imeendelea kutesa kwa kupata ushindi na safari hii wakicheza bila nyota wao Kylia Mbappe aliyeambukizwa virusi vya Corona, jana wameweza kuwafunga Croatia magoli manne kwa bila goli moja likifungwa kwa njia ya Penalti na Oliver Giroud. Ureno ambayo iko kundi moja na Ufaransa, sasa inaongoza kundi hilo baada ya kuishinda Sweden. Hiyo ni mechi ya pili mfululizo kwa Sweden kupoteza, na ni mechi muhimu kwa Ronaldo ambaye ameweka rekodi ya kufunga goli la 100 katika mashindano ya kimataifa. Anakuwa mchezaji wa kwanza wa Ulaya kufikisha magoli 100 kwenye mechi ya kimataifa. Anayeshikilia rekodi hiyo kwa sasa ni Ali Daei wa Iran aliyeifungia timu yake magoli 109.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako