• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yasema ukusara wa tovuti uliotolewa na Marekani kuhusu Xinjiang ni wa kueneza uongo na uvumi

  (GMT+08:00) 2020-09-15 09:07:47

  Wizara ya mambo ya nje ya Marekani tarehe 13 kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter ilitangaza kutoa ukurasa wa tovuti kuhusu Xinjiang, China. Msemaji wa wizara hiyo Bi. Morgan Ortagus siku hiyo pia kwenye Twitter alitoa kauli zisizo za haki kuhusu suala la Xinjiang.

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Wang Wenbin jana amesema, ukurasa huo wa tovuti uliotolewa na wizara ya mambo ya nje ya Marekani una lengo la kueneza uongo na uvumi, na kuficha ukweli.

  Bw. Wang amesema Marekani imefumbia macho ukweli wa maendeleo ya Xinjiang, nia halisi ya Marekani sio kujali hali ya haki za binadamu, bali ni kutumia kile inachokiita "masuala ya haki za binadamu" kuharibu ustawi na utulivu wa Xinjiang na kuzuia maendeleo ya China.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako