• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TikTok yawasilisha pendekezo la kusuluhisha hofu ya usalama kwa mamlaka nchini Marekani

    (GMT+08:00) 2020-09-15 16:48:04

    Kampuni ya mtandao wa kijamii wa TikTok imesema imewasilisha pendekezo kwa uongozi wa Marekani litakalosaidia kusuluhisha wasiwasi wa kiusalama wa nchi hiyo.

    Kampuni hiyo yenye makao yake makuu jijini Los Angeles, imesema katika taarifa yake kuwa, inaweza kuthibitisha kuwa imewasilisha pendekezo hilo kwa Wizara ya Fedha nchini Marekani, na kuongeza kuwa hatua hiyo itasaidia utendaji wa kampuni hiyo katika siku za baadaye.

    Taarifa hiyo pia imesema, pendekezo hilo litawasaidia kuendelea kuunga mkono jamii yake ya watu milioni 100 nchini Marekani wanaopenda kutumia TikTok kwa ajili ya mawasiliano na kujiburudisha, na maelfu ya wamiliki wa biashara ndogo na wabunifu ambao wanategemea TikTok kukuza kipato chao na kujenga ajira za uhakika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako